Friday, December 25, 2020

TELEGRAM KUANZISHA MATANGAZO 2021


Muanzilishi wa Telegram - Pavel Durov amesema Telegram imekuwa ikitoa huduma zake kwa kutegemea michango ya wadau mbalimbali bila kutengeneza faida yoyote. 

Pavel amesema kuwa Telegram itaanza kuweka matangazo katika channels ambazo zinawashirikisha wadau mbalimbali na pia itatambulisha mfumo wa stickers ambazo zitauzwa na watumiaji wanaweza kuzibadilisha na kiasi cha fedha na kupata pesa. Pia watengenezaji wa Stickers na Admins wa Channels za Telegram watapata faida kwa kugawana na Telegram faida ya matangazo. Matangazo yatakuwa yanafanana na style ya messages ili muonekano usibadilike sana na mfumo wa Matangazo utamilikiwa na Telegram.

Telegram imesema haitaweka matangazo yoyote katika chats za watu ili kuondoa usumbufu na wabunifu wa stickers watalipwa. Huu ndio muda wa kutengeneza Public Channels ambazo zitadumu ili kupata kipato kutoka katika matangazo kwenye miaka ijayo.

Telegram sio ya kwanza kulalamika kuwa haipati faida; WhatsApp imekuwa ikijaribu pia kuweka matangazo katika WhatsApp Beta ya majaribio na Facebook imesema inapata hasara katika kusimamia platform yake ya WhatsApp ambayo haiingizi kipato chochote. Kwa Telegram itakuwa ni njia ya kuipa uhuru wa kuwa na usalama kwa sababu iliwahi kulalamikiwa inatoa data zake kwa wadhamini wake! Unaonaje mpango huu wa Telegram?
 

OnePlus 9Pro Kuzinduliwa 2021


 Pete Lau ambaye ni CEO wa OnePlus, amethibitisha tetesi zinazohusu ujio wa Smartwatch ya kwanza kutengenezwa na OnePlus. Mwezi wa tatu mwakani 2021, OnePlus 9 na OnePlus 9Pro zitatambulishwa rasmi na inategemewa OnePlus itatangaza Smartwatch zake. 

OnePlus na Oppo zipo chini ya kampuni moja na Oppo mwanzoni mwaka huu ilitoa saa yake ya kwanza japo ilipingwa sana kwa kutumia mfumo wa Google (mfumo wa Wear OS). Let’s see tech mpya ambayo OnePlus itakuja katika kupambana na soko la Apple, Xiaomi na Google na Samsung.

TANZIA:Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza afariki Dunia .


 Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mngereza afariki Dunia . Taarifa za kifo Chake zimethibitishwa Usiku huu na Watu wa Karibu yake huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijawekwa wazi . tunatoa Pole kwa Familia yake, Wasanii na Watanzania kwa ujumla kwa Msiba huu Mzito kwa Taifa . Tutamkumbuka Daima Mh. Mngereza kwa kujitoa kwake na Jitihada zake za kuhakikisha Sanaa ya Tanzania inasonga mbele . Mungu ailaze Roho yake Mahala Pema Peponi AMIN

Tuesday, July 7, 2015

EIJI TSUBURAYA.


Leo katika historia anakumbukwa mtayarishaji mkubwa wa filamu kwa jina anaitwa
Eiji Tsuburaya ambaye alizaliwa: julai 7 1901(Sukagawa, Fukushima) huko japan.
na kufariki januari 25 1970.
Anakumbukwa kutokana na kipaji chake cha uwongozaji wa picha za kusisimua(special effects)
ni mwanzilishi wa filamu ya Godzila na ultraham.

Saturday, July 4, 2015

Maneno ya Mustafa baada ya TV za Kenya kupigwa marufuku .

Maneno ya Mustafa baada ya TV za Kenya kupigwa marufuku .

ColonelBaada ya video kama za ‘Nishike’ ya Sauti Sol na ‘You guy’ ya P Unit kufungiwa, headlines za sasa zimeangukia kwa Mustafa Colonel ambaye ni siku za karibuni tu alishikwa na Polisi kwa madai kuwa kwenye hii video kuna Mwanamke ambaye ni nyumba ndogo ya kigogo flani hivyo picha alizopigwa hazitakiwi kuvuja.
Baada ya hayo video ilipotoka kwa ubishi bila picha kufutwa, imefungiwa kuonyeshwa kwenye TV za Kenya kwa sababu imevuka mipaka ya kuzingatia maadili
Shamsa aliripoti Polisi baada ya kutishiwa maisha na mchumba wake

Shamsa aliripoti Polisi baada ya kutishiwa maisha na mchumba wake

Muigizaji wa filamu Shamsa Ford amefunguka na kusema kwamba tangu aachane na Ex boyfriend wake Dickson Matoke aliwahi kuwatishia kuwauwa yeye na mwanae zaidi ya mara 10.
Akizungumza na millardayo.com alisema…’Ni kweli wakati nilipokuwa katika mahusiano naye alikuwa ni mtu ambaye anapenda sana kuniambia neno nitakuuwa mimi na mwanangu ndio maana nilikuwa naogopa sana kwasababu nilihisi kuwa anaweza kufanya lolote kunikomoa na nilienda hadi polisi kuchukua RB yake ili kama lolote litakalotokea basi yeye atakuwa amehusika, yaani yule alikuwa ananiambia kabia yuko serious mbaya kuwa ataniuwa mimi na mtoto wangu lisha kwangu alikuwa anawaambia hata marafiki zangu ni mashahidi na mbaya zaidi alikuwa anasema hayo maneno na mbaya zaidi alikuwa anawaambia hata ndugu zake.
.
Shamsa Ford akiwa na Ex Boyfriend wake Dickson Matoke Enzi hizo wa uhusiano wao.
Hayo maneno alikuwa anayaongea wakati bado niko naye kwenye uhusiano lakini ndio hivyo malumbano malumbano na mimi nilikuwa nimeshachoka na hizo tabia zake lakini baada ya kuachana naye ni vitisho labda anataka kumuona mtoto anatumia vitisho mara sasa ninapomnyima mtoto basi anatumia vitisho basi mimi nikikumbuka lile neon lake la kusema ataniuwa basi moyoni sina amani….’alisema.

Tuesday, June 30, 2015

FACEBOOK KUAMIA AFRIKAH KUSINI.

FACEBOOK KUAMIA AFRIKAH KUSINI.

Facebook-Headquarters
Nimeipata hii takwimu ambayo sikuwa nafahamu, kumbe Facebook ina watumiaji Milioni 120 wa Mtandao huo ndani ya Africa pekeyake !!
Story nyingine kuhusu Facebook kwa sasa hivi ni ishu ya kusogeza Office zao mpaka ndani ya Jiji la Johannesburg Afrika Kusini na tayari hapo ndio yatakuwa Makao Makuu ya shughuli zao zote zinazohusu Facebook Afrika, Nunu Ntshingila ndio Boss ambaye kachukua ajira kusimamia Kampuni hiyo.
enter-facebook-office
Mark Zuckerberg, Boss wa Facebook
Kingine ni kwamba jamaa wameamua kuisogeza Facebook ndani ya Afrika kama njia ya kusogea karibu ya wateja wao wengi ambao ni Wafanyabiashara wanaotumia Mtandao huo katika kutangaza biashara zao.
Facebook-opens-first-African-o
Facebook iliangalia siku nyingi sana jinsi ya kuingia kwenye soko la Afrika, waliwahi kurahisisha huduma kwa watumiaji wa mtandao huo kwa kuweka App maalum ambayo mtumiaji hakatwi pesa wala hatumii data kwenye kuchat, mpango wao mwingine ni kuhakikisha wanamfikia kila mtu hata ambae hana uwezo wa kumiliki simu yenye uwezo wa Internet.
1200x-1
Nunu Ntshingila, Boss wa Facebook Afrika.
Mpango walionao kwa sasa ni kuajiri wafanyakazi 25 ili ofisi ya Johannesburg ijitosheleze na kazi iendelee kama kawaida