Friday, December 25, 2020

TELEGRAM KUANZISHA MATANGAZO 2021


Muanzilishi wa Telegram - Pavel Durov amesema Telegram imekuwa ikitoa huduma zake kwa kutegemea michango ya wadau mbalimbali bila kutengeneza faida yoyote. 

Pavel amesema kuwa Telegram itaanza kuweka matangazo katika channels ambazo zinawashirikisha wadau mbalimbali na pia itatambulisha mfumo wa stickers ambazo zitauzwa na watumiaji wanaweza kuzibadilisha na kiasi cha fedha na kupata pesa. Pia watengenezaji wa Stickers na Admins wa Channels za Telegram watapata faida kwa kugawana na Telegram faida ya matangazo. Matangazo yatakuwa yanafanana na style ya messages ili muonekano usibadilike sana na mfumo wa Matangazo utamilikiwa na Telegram.

Telegram imesema haitaweka matangazo yoyote katika chats za watu ili kuondoa usumbufu na wabunifu wa stickers watalipwa. Huu ndio muda wa kutengeneza Public Channels ambazo zitadumu ili kupata kipato kutoka katika matangazo kwenye miaka ijayo.

Telegram sio ya kwanza kulalamika kuwa haipati faida; WhatsApp imekuwa ikijaribu pia kuweka matangazo katika WhatsApp Beta ya majaribio na Facebook imesema inapata hasara katika kusimamia platform yake ya WhatsApp ambayo haiingizi kipato chochote. Kwa Telegram itakuwa ni njia ya kuipa uhuru wa kuwa na usalama kwa sababu iliwahi kulalamikiwa inatoa data zake kwa wadhamini wake! Unaonaje mpango huu wa Telegram?
 

Related Posts

TELEGRAM KUANZISHA MATANGAZO 2021
4/ 5
Oleh

Subscribe via email

Like the post above? Please subscribe to the latest posts directly via email.